SUPASTAA wa soka, Mario Balotelli,
amesema ataanza kufanyia kazi suala la kupunguza jazba ndani ya uwanja
ili kunusuru maisha yake ndani ya San Siro
Fowadi huyo wa AC Milan, amesema dhamira yake kwa
sasa ni kuhimili purukushani zote za ndani ya uwanja ili kukwepa adhabu
zinazoepukika ambazo zimekuwa zikiigharimu klabu yake.
Straika huyo amehusishwa na matukio mengi ya utovu
wa nidhamu ndani ya uwanja msimu huu na hivi karibuni alidaiwa
kulumbana na Nicolas Spolli juu ya suala la kibaguzi kwenye mechi dhidi
ya Catania, licha ya kwamba beki huyo alisafishwa kwamba hakufanya tukio
lolote la ajabu.
Baada ya kuona mambo yanazidi kumwandama, staa huyo wa zamani wa Manchester City, ameahidi kubadili tabia na kwamba atakuwa mchezaji mwenye nidhamu kubwa ndani ya uwanja hasa akizingatia dhamira yake ni kubaki kuwa mchezaji wa AC Milan.
“Ukilinganisha na miaka ya nyuma, mambo mengi sana
yamebadilika. Nitaendelea kubadili tabia. Lakini, kubwa nitaendelea
kubaki hapa,” alisema.
Balotelli alisifu mbinu za makocha wake
wanazotumia kwa sababu zimemfanya kuwa tofauti hadi kufikia sasa kwenye
maisha yake ya soka na anasisitiza kwamba ataendelea kuboresha na
kupandisha kiwango chake kiuchezaji.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!