SHIRIKISHO la Kimataifa la Soka (Fifa)
limeipa Tanzania mgawo wa tiketi 260 za fainali za Kombe la Dunia
zitakazochezwa Brazil mwakani.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la
Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema Watanzania wanaohitaji tiketi
hizo wanatakiwa kutuma maombi TFF kwa maandishi wakielezea aina ya
tiketi na mechi wanazotaka kushuhudia.
Alisema hakuna tiketi zitakazotolewa pasipo maombi
ya maandishi na tiketi zilizopo Tanzania ni kwa hatua ya makundi,
raundi ya 16 bora, robo fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.
“Kwa mechi ya ufunguzi, nusu fainali mbili na
fainali (mechi namba 1, 61, 52 na 64) ni tiketi kumi tu ndizo
zitakazopatikana na bei za tiketi ziko katika viwango vitatu tofauti,”
alisema.
“Mechi ya ufunguzi tiketi zake ni dola za Marekani 495, 330 na 220.
Hatua ya makundi (mechi namba 2-48) ni dola 175, 135 na 90 na hatua ya 16 bora (mechi namba 49-56) ni dola 220, 165 na 110.
“Robo fainali (mechi namba 57-60) ni dola 330, 220
na 165 wakati nusu fainali (mechi namba 61 na 62) ni dola 660, 440 na
275 na mechi ya mshindi wa tatu ni dola 330, 220 na 165 wakati kiingilio
kwa fainali kitakuwa dola 990, 660 na 440.”
Alisema TFF itawasilisha maombi ya tiketi hizo
Fifa kuanzia Desemba 8 mwaka huu hadi Februari 7 mwakani na idadi ambayo
itaombwa itatokana na Watanzania watakaowasilisha maombi TFF.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!