Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » Ndege zisizokuwa na rubani kuanza operesheni za usalama Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,DRC

Ndege zisizokuwa na rubani kuanza operesheni za usalama Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,DRC

Written By Unknown on Monday, 2 December 2013 | Monday, December 02, 2013

Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza utatumia ndege zisizokuwa na rubani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo kesho Jumanne, kusaidia kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Rwanda na kuchunguza makundi ya waasi baada ya lile la M 23 kusambaratishwa.

Kwa mara ya kwanza ndege zisizokuwa na rubani kutoka Italia ndizo ambazo zimechaguliwa na Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi na kuimarisha hali ya utulivu katika eneo la Mashariki mwa DRC.
Hatua ya Umoja wa Mataifa imelenga kufuatilia harakati za makundi ya uasii katika maeneo ya Kivu, wakati huu kukiwa na taarifa kuhusu raia kukimbia makazi wakielekea katika mpaka wa DRC na Rwanda.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Shughuli hizo za ufuatiliaji lazima zifanyike kwa ndege hizo zisizokuwa na rubani kutokana na uwezo wa ndege hizo kuweza kuruka kwa muda mrefu, mchana na usiku, kwa gharama ya chini sana.
Mkuu wa oparesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa Herve Ladsous, amesema operesheni hii imelenga kuzuia uhalifu wa aina yoyote kuzuka na kuongeza kuwa ndege tano zisizokuwa na rubani zitapelekwa katika maeneo ya Kivu kuhakikisha ufuatiliaji kwa masaa 24.
Wachambuzi wa masuala ya usalama wanaona kuwa hatua hii ni nzuri ingawa viongozi wa mataifa ya ukanda husika huenda wakaikosoa kwa kuona pengine nia ya Marekani ni kuzichunguza nchi jirani na DR Congo.
Katika hatua nyingine Raisi wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo,Joseph Kabila ametangaza kusitisha kwa muda ziara yake mashariki mwa nchi hiyo na sasa ataelekea mjini Kampala Uganda kwa mazungumzo na raisi wa taifa hilo Yoweri Kaguta Museveni kuhusu hatma ya mazungumzo ya Kampala baada ya kusambaratishwa kwa kundi la waasi wa M23.
Mwezi mmoja uliopita vikosi vya serikali ya DRC kwa kusaidiwa na vile vikosi maalum vya Umoja wa Mataifa vilivyoko mashariki mwa nchi hiyo walifanikiwa kuwafurusha waasi wa kundi la M23 waliokuwa wakikalia maeneo mengi ya mashariki ya nchi hiyo.
Kabla ya kuondoka mjini Goma raisi Kabila amewaomba raia wa eneo hilo kuwa na subira na serikali yake inajipanga upya kuanza utekelezaji wa miradi ya maendeleo baada ya kulishinda kundi la M23.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi