Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » NAMISS SANA KUNDI LETU LA WAKILISHA NA MMISS SANA MAREHEMU LANGA NA WITNESS:SHAA

NAMISS SANA KUNDI LETU LA WAKILISHA NA MMISS SANA MAREHEMU LANGA NA WITNESS:SHAA

Written By Unknown on Saturday, 28 December 2013 | Saturday, December 28, 2013

Member wa zamani wa kundi la WAKILISHA, Sara Kaisi aka Shaa wa Sugua Gaga ameelezea jinsi ambavyo analimiss kundi hilo lilokuwa likiundwa na Witness, marehemu Langa na yeye (Shaa).
Shaa alisema kuwa alipokuw na kundi hilo mambo yalikuwa mepesi zaidi kwake kwa upande wa utendaji kazi.
Shaa alikuwa anakabidhiwa tu kazi ya kuweka vocal na kuelekezwa baadhi ya sehemu na kutisha kwenye ngoma hizo.  
“Enzi za Wakilisha unajua tulikuwa bado wadogo, halafu mimi ndio ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuwa kwenye soko la muziki. Kwa hiyo nilikuwa sijui kuandika nilikuwa naandikiwa saa zingine na Witness, saa zingine na Langa, saa zingine ilikuwa ni manager wetu ambaye alikuwa Daniel Kiondo.
“Nilikuwa directiwa yaani, ilikuwa nikiingia ni ile haya fanya hivi pita hapa, ilikuwa rahisi sana. Tukipanda stejini tuko watatu, sio lazima mimi ndio  nipige kelele ‘changamsha audience nini’, hiyo namiss ile mbaya.”Alisema Shaa.
Mwimbaji huyo aliunganisha kipindi hicho alipokuwa na Wakilisha na kipindi hiki ambacho anafanya kazi peke yake.
Lakini sasa hivi nikipanda stejini sasa hivi kama Shaa, uko mwenyewe macho yote kwako. Ukiingia studio kama ni wimbo ni wako wewe ndio uandike na wewe ndio uamue.  Ilikuwa inasaidia tukiwa watatu kazi zinaenda smooth, sasa hivi ukiwa mmoja inabidi uumize kichwa zaidi. Hicho ndicho nakimiss upande wa kazi.”

Shaa ameimiss company ya kawaida ya rapper wa kike Witness na marehemu Langa ikiwa ni pamoja story za kishikaji.
“Upande wa ushikaji, namiss kusema ukweli u-closeness wetu, urafiki wetu. Ile kwamba baada ya show au kama hakuna show tunachill tu sehemu tunapiga story, tunateta idea za nyimbo, au bwana umesikia story ya flani ‘amefanya nini’, aaah, balaaa..nini. Kwa hiyo ule tu ushikaji nimeumiss sana. Rest in peace Langa, nimemmiss sana.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi