ARSENE Wenger amesifu kiwango cha timu
yake ya Arsenal cha kupambana kutoka nyuma na kisha kuichapa West Ham
United mabao 3-1 kwenye Ligi Kuu England juzi Alhamisi na kusema sasa
wamerudi kuwashika kwenye mbio za ubingwa.
Arsenal imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo
baada ya ushindi huo uliokuwa wa kwanza kwao katika mechi nne
zilizopita. Liverpool iliyokuwa kileleni imeporomoka hadi nafasi ya nne
baada ya kichapo kutoka kwa Manchester City ambayo kwa sasa imeshika
nafasi ya pili ikiwa na pointi 38, moja pungufu ya vinara Arsenal.
Katika mechi yake, Arsenal ilianza kufungwa kwa
bao la Carlton Cole, lakini nyota wake Theo Walcott alifunga mara mbili
kabla ya majeruhi kwa muda mrefu, straika wa Kijerumani, Lukas Podolski,
kurejea uwanjani na neema baada ya kufunga bao la tatu katika kipindi
cha pili.
“Tumetoa jibu la maswali yetu,” alisema Wenger mara baada ya ushindi huo.
“Kama tusingeshinda kungekuwa na maswali mengi
sana juu yetu. Hii ilikuwa ni mechi ambayo tusingeshinda ingekuwa balaa.
Kwa kiwango hiki tumeonyesha sasa ni washindani. Timu inafanya vizuri
na fikira zetu siku zote ni kuketi kileleni.”
Baada ya ushindi huo Arsenal sasa mtihani wake ujao ni kuivaa Newcastle United kwenye Uwanja wa St James’ Park kesho Jumapili.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!