KOCHA Mkuu wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson,
juzi Alhamisi alikuwa kivutio kwenye Uwanja wa KC wakati wa mchezo wa
Ligi Kuu England dhidi ya Hull City kwa kukaa kwenye benchi la wachezaji
wa akiba huku akiwa ametinga sare za timu hiyo.
Benchini hapo, Ferguson alikuwa amevaa koti na tai
zenye nembo ya klabu ya Manchester United na kuketi sambamba na
wachezaji wa akiba akiwamo winga Wilfied Zaha.
Kwenye mchezo huo, Manchester United iliduwazwa
kwa mabao mawili ya haraka, lakini uwepo wa Ferguson uliwatoa hofu
wachezaji na kocha wao, David Moyes na hivyo kupambana na kuibuka na
ushindi wa mabao 3-2 uliowafanya kupanda kwa nafasi moja kwenye msimamo
kutoka ya nane hadi namba saba.
Baada ya mabao hayo ya Hull City yaliyofungwa na
James Chester na David Meyler, presha ilionekana kuwa kubwa kwa kocha
mpya, Moyes hasa ukizingatia mtangulizi wake alikuwa kwenye benchi,
lakini mabao ya Chris Smalling, Wayne Rooney yalinusuru mambo kabla ya
Chester kujifunga na kuifanya Manchester United kuzidi kufufua ndoto za
kutetea ubingwa.
Miamba hayo wa Old Trafford wanashika nafasi ya
saba kwenye msimamo, pointi nane nyuma ya vinara Arsenal wanaoongoza na
pointi zao 39.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!