BEKI wa kati wa Manchester City, Vincent Kompany, amesema kama
kuna jambo alilolipenda ndani ya uwanja kwenye mechi dhidi ya Liverpool
ni usumbufu wa straika, Luis Suarez.
Kompany alikuwa na shughuli pevu ya kumtuliza
straika huyo kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu England wakati Manchester
City ilipomenyana na Liverpool juzi Alhamisi.
Mchezo huo ulimalizika kwa Manchester City
kuichapa Liverpool mabao 2-1 na kuwashusha kileleni mwa msimu wa ligi
hiyo, huku vijana hao wa Manuel Pellegrini wakiendelea kufurahia rekodi
nzuri kwenye uwanja wao wa nyumbani, Etihad.
Lakini, kitendo cha kupambana na fowadi hatari na
anayetumia ujanja sana anapokuwa uwanjani kimemfurahisha Kompany, ambaye
pia ni nahodha wa Manchester City.
“Nilipenda kila sekunde niliyopambana na Suarez. Ni straika mjanja sana na ilikuwa safi kukabiliana naye,” alisema Kompany.
“Baada ya mechi tulishikana mikono na aliikubali vita yetu nami niliikubali pia. Tumeshinda, ila ilikuwa mechi ngumu sana.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!