Uchunguzi mpya unaonyesha kuwa, jumla ya watu milioni 18 nchini
Uingereza wanaishi kwa wasi wasi mkubwa kutokana na kipato duni cha
fedha. Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliofanywa na Shirika linalojihusisha
na viwango vya ununuzi wa bidhaa muhimu MoneySupermarket.com, imeelezwa
kuwa masuala ya kipato dunia cha fedha ni miongoni mwa mambo ambayo
yamekuwa yakiwatia wasi wasi mkubwa raia wengi wa Uingereza sanjari na
kuathiri pia usalama nchini humo. Ripoti hiyo imeeleza kuwa, jumla ya
asilimia 52 ya watu walioshirikishwa katika uchunguzi huo, walisema
kuwa, kwa muda mrefu au hatua kwa hatua wamekuwa wakikabiliwa na hali
ngumu ya kifedha na kwamba wanawake ndio waathirika zaidi kuhusiana na
tatizo hilo. Uchunguzi huo pia umebaini kuwa, asilimia 19 ya watu wazima
nchini Uingereza wanafahamu kuwa, hali mbaya ya uchumi unaoikabili nchi
hiyo hivi sasa ndio chanzo cha mfadhaiko wa moyo na wahka vinavyo
wakabili watu wengi nchinio. Mbali na hapo asilimia 75 ya washiriki wa
uchunguzi huo, wamesema kuwa hali mbaya ya kipato cha fedha itashadidi
zaidi katika mwaka ujao wa 2014.
Home »
siasa kimataifa
» MAMILIONI YA WATU WADAIWA KUWA NA MAISHA MAGUMU NCHINI UINGEREZA
MAMILIONI YA WATU WADAIWA KUWA NA MAISHA MAGUMU NCHINI UINGEREZA
Written By Unknown on Sunday, 29 December 2013 | Sunday, December 29, 2013
Labels:
siasa kimataifa
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!