Msemaji wa tume ya utetezi wa aliyekuwa rais wa Misri Muhammad Mursi na
kiongozi wa Ikhwanull Muslimin katika faili la matukio ya ikulu ya
Ittihaadiyyah nchini humo, ametangaza kuwa, leo tume hiyo itawasilisha
ombi lake rasmi la kutaka kuainishiwa muda wa kukutana na mteja wao
huyo. Muhammad Ad-Damati amesema kuwa, lazima tume hiyo ikutane na rais
huyo aliyeuzuliwa madarakani na jeshi la nchi hiyo kabla ya tarehe ya
kufikishwa kwake mahakamani. Mursi anatuhumiwa kuhusika katika matukio
ya ikulu ya Ittihaadiyyah yaliyopelekea kuuliwa watu watatu kati ya
waandamanaji na halikadhalika kufanya ujasusi kwa ajili ya Harakati ya
Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na hadi sasa anaendelea
kushikiliwa na jeshi la nchi hiyo katika jela ya Burj al-Arab ya mkoa wa
Alexandria nchini humo. Aidha rais huyo wa zamani wa Misri anatarajiwa
kupandishwa kizimbani, mnamo tarehe 8 Januari mwakani. Hayo yanajiri
katika hali ambayo hali ya machafuko bado vinaendelea kushuhudiwa nchini
Misri ambapo hapo jana machafuko na uchomaji moto vilishuhudiwa Chuo
Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar kati ya jeshi na wanafunzi wanaomuunga
mkono Mursi. Mbali na hapo pia jana watu watano waliripotiwa kuuawa na
makumi ya wengine kujeruhiwa katika mapigano yaliyozuka kati ya askari
usalama na wafuasi wa Muhammad Mursi Rais halali wa nchi hiyo
aliyepinduliwa na jeshi mwezi Julai mwaka huu.
Home »
» TUTAKUTANA NA RAIS MURSI GEREZANI:TUME YA UTETEZI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!