Wanawake Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar, wanakabiliwa na
vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na maafisa usalama katika
vituo vya polisi nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti maafisa wa usalama
nchini Myanmar wamekuwa wakiwateka nyara wanawake na wasichana Waislamu
wa kabila hilo sanjari na kuwapiga na kuwatukana.
Habari zinasema kuwa, baada ya maafisa hao kuwalazimisha kutumia madawa ya kulevya huwapeleka katika vituo vya usalama na kuwabaka bila ya wao kujielewa. Hii ni katika hali ambayo jamii ndogo ya Waislamu nchini humo imekuwa ikinyimwa haki zake za kimsingi kutokana na serikali ya Naypyidaw kupinga kuwapa Waislamu wa jamii hiyo haki yoyote kwa madai kuwa eti sio raia wa nchi hiyo. Aidha kwa mara kadhaa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakiituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia vimavyofanywa na maafisa wa usalama na jeshi dhidi ya wanawake Waislamu wa kabila la Rohingya nchini humo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!