Jacqueline Zwambila balozi wa Zimbabwe nchini Australia |
Zwambila alisema kuwa, hawezi kurejea nchini humo kutokana na hatari inayoweza kuyakabili maisha yake. Aidha akishiria matamshi hayo ya Zwambila, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zimbabwe Kembo Mohadi, ameongeza kuwa, hadi sasa viongozi wote wa chama cha upinzani cha MDC wanaishi nchini humo huku wengine wakiwa wanatekeleza majukumu yao kama wabunge serikalini na hakuna hatari yoyote inayowakabili. Hivi karibuni balozi huyo wa Zimbabwe nchini Australia aliomba hifadhi ya ukimbizi nchini humo kwa madai kwamba, haoni sababu ya kurejea nyumbani baada ya chama cha ZANU PF nchini Zimbabwe kufanya udanganyifu mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 31 Julai mwaka huu na kwamba, maisha yake yatakuwa hatarini iwapo atarejea nchini humo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!