"Naamini watu zaidi ya milioni 3 watashiriki kwenye maandamano ya leo. Kama Yingluck hatajiuzulu, tutaendelea na maandamano, leo tunasimamisha mawasiliano ya barabarani kwa nusu siku, na safari nyingine tutasimamisha kwa siku nzima."
Lakini takwimu za polisi zimesema, idadi ya waandamanaji ilifikia laki 1.5.
Maandamano ya mara kwa mara yamekuwa yakishuhudiwa nchini Thailand katika miezi miwili iliyopita. Hapo awali waziri mkuu Bibi Yingluck alivunja bunge kujibu matakwa ya waandamanaji, na kutangaza siku ya uchaguzi, lakini waandamanaji hawakuridhika na matokeo hayo na kutaka Bibi Yingluck mwenyewe kujiuzulu na kuahirisha uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Februari mwakani ili kupata muda wa mwaka mmoja na nusu wa kujindaa kwa uchaguzi mkuu na kufanya mageuzi.
Hata hivyo, tume ya uchaguzi wa nchi hiyo imesisitiza kuwa uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuanza leo hautaahirishwa. Lakini wakati huohuo watu wa hali mbalimbali ya jamii ya Thailand wameeleza matakwa yao ya kutaka mageuzi yafanyike. Chama kikubwa zaidi cha upinzani cha Demokrasia kimeamua kususia uchaguzi mkuu ujayo, kama anavyoeleza kiongozi wa chama hicho Bw Abhisit Vejjajiwa.
"Tumeamua kutoshiriki kwenye uchaguzi wa mwakani. Ningependa kuwaambia wananchi wanaotaka kukipigia kura chama cha Demokrasia, kwamba mageuzi ambayo mngependa kuyaona yatatimizwa, na siku hiyo itakapofika, tutafanya mageuzi ya muda mrefu na kurudisha imani ya wananchi juu ya demokrasia na mfumo wa bunge. Haya ndiyo matumaini ya chama cha Demokrasia. Tumefanya uamuzi huu na tutaendelea nao."
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!