Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Iran Bi. Marzieh Afkham amelaani vikali shambulio la kigaidi
lililolenga kanisa moja katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad. Akizungumza
Jumatano, Afkham ametoa salamu za rambi rambi za Jamhuri ya Kiislamu kwa
familia za waliopoteza maisha na waliojeruhiwa.
Amesema kitendo hicho kinapasa kutoa
msukumo kwa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na vitendo viovu
vya ugaidi na misimamo ya kufurutu ada. Ameongeza kuwa hujuma dhidi ya
kanisa na waliomo ndani ya jengo hilo la ibada ni kengele ya hatari kuwa
ugaidi hauna mipaka ya kijiografia, kidini au kimadhehebu. Kwa uchache
watu 37 waliuawa na zaidi ya wengine 50 kujeruhiwa katika mashambulio ya
mabomu yaliyolenga maeneo ya Wakristo mjini Baghdad hiyo jana. Hakuna
kundi lolote lililodai kuhusika na mashambulio hayo lakini wataalamu
wanasema hujuma kama hizo kwa kawaida hutekelezwa na magaidi wenye
mfungamano na mtandao wa al-Qaeda.
Umoja wa Mataifa unasema karibu watu 8,000 wamepoteza maisha mwaka 2013 nchini Iraq kutokana na mashambulio ya kigaidi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!