Taasisi ya Al Aqsa imeonya kuhusu njama zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana
Jumatano na Taasisi ya Waqfu na Turathi ya Al Aqsa, utawala wa Israel,
bunge la utawala huo Knesset pamoja na vibaraka wao, kila siku
wanazidisha njama za kuuharibu Msikiti wa Al Aqsa.
Taarifa hiyo imesema Msikiti wa Al Aqsa
ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu unapasa kutumiwa na Waislamu tu.
Taarifa hiyo imesema kuwa Bunge la Israel, Knesset, siku ya Jumanne
liliitisha kikao maalumu kuhusu uendeshaji wa Idara ya Waqfu wa
Kiislamu, Baitul Muqaddas. Utawala wa Kizayuni wa Israel tokea uikalie
kwa mabavu Baitul Muqaddas umekuwa ukichimbua maeneo yaliyoko karibu na
Msikiti wa Al Aqsa kwa lengo la kuuharibu kabisa msikiti huo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!