Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SHIRIKA MOJA LA UFARANSA LAPINGWA NA MAMIA YA WA NIGERIA HADI KUINGIA BARABARANI KUANDAMANA

SHIRIKA MOJA LA UFARANSA LAPINGWA NA MAMIA YA WA NIGERIA HADI KUINGIA BARABARANI KUANDAMANA

Written By Unknown on Sunday, 22 December 2013 | Sunday, December 22, 2013

Mamia ya raia nchini Nigeria wamefanya maandamano kupinga kutekelezwa mapatano yasiyo na mlingano kati ya nchi yao na Shirika la Kifaransa la Arva. Maandamano hayo yaliyowajumuisha wafanyakazi, wanafunzi wa vyuo vikuu, waandishi wa habari, wanasiasa na viongozi wa taasisi zisizo za kiserikali, yalifanyika jana mbele ya bunge la Nigeria na karibu na ofisi ya shirika hilo la Ufaransa. Waandamanaji walishindwa kufika ofisi za Arva baada ya polisi kuweka uzio karibu na ofisi za shirika hilo.
Mmoja wa waratibu wa maandamano hayo Bwana Ali Idris amesema kama ninavyomnukuu: “Kwa miaka 45 sasa Ufaransa imekuwa ikishirikiana na viongozi wa Nigeria katika kupora madini ya uran ya nchi yetu.” Mwisho wa kunukuu. Aidha mwana harakati huyo ameongeza kwa kusema kuwa, karibu lampu 35 kati ya 100 nchini Ufaransa, zinawaka kwa urani ya Nigeria huku raia wa Nigeria wenyewe wakiendelea kutumia kuni. Amesema kuwa, mikataba yote iliyowekwa kati ya serikali ya Abuja na  Shirika la Arva la Ufaransa, haina mlingano wowote. Kati ya asilimia 70 ya madini ya urani yanayozalishwa nchini Nigeria, asilimia 5 tu ya madini hayo ndio hubakia nchini humo. Raia wa Nigeria wanataka kubatilishwa mikataba hiyo kati ya serikali na shirika hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi