Leo ni Jumapili tarehe 19 Mfunguo Tano Safar 1435 Hijria sawa na tarehe 22 Disemba mwaka 2013 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 2159 iliyopita, duru ya tatu na ya mwisho ya vita vya kihistoria na vya umwagaji damu kati ya tawala za kifalme za Carthage na Roma ilimalizika kwa kupata ushindi Waroma na kuanguka utawala wa Wacartharge. Vita vya falme hizo mbili vilijulikana kwa jina mashuhuri la vita vya Punic. Utawala wa kifalme wa Carthage ulikuwa moja kati ya tamaduni kongwe huko kaskazini magharibi mwa Afrika na katika pwani ya bahari ya Mediterrania.
Siku kama ya leo miaka 374 iliyopita alizaliwa Jean Racine malenga na mwandishi wa michezo ya kuigiza wa Kifaransa. Racine alianza kazi ya uandishi baada ya kujisomea kwa muda fulani na katika ujana wake alipata umashuhuri kutokana na kuandika mchezo wa tanzia alioupa jina la Andromaque.
Siku kama ya leo miaka 320 iliyopita, ulitokea mtetemeko mkubwa wa ardhi katika kisiwa cha Sicily kusini mwa Italia. Kufuatia zilzala hiyo, miji mitatu mikubwa ya kisiwa hicho iliteketezwa na kusababisha hasara kubwa kwa miji mingine yakiwemo makao makuu ya kisiwa hicho yaani Palermo. Mtetemeko huo wa ardhi unahesabiwa kuwa mtetemeko mkubwa zaidi wa ardhi kuwahi kutokea nchini Italia. Zaidi ya watu elfu themanini walipoteza maisha yao kufuatia janga hilo la kimaumbile.
Na siku kama ya leo miaka 57 iliyopita, Ufaransa na Uingereza zilihitimisha udhibiti wao wa siku 50 dhidi ya bandari ya Port Said ya nchini Misri na kutoa majeshi yao katika bandari hiyo. Inafaa kuashiria hapa kwamba, baada ya utawala haramu wa Israel kufanya mashambulio katika jangwa la Sinai, mashambulio ya pamoja ya anga ya Uingereza na Ufaransa dhidi ya Misri nayo yalianza. Mashambulio hayo, yalipelekea kutokea hasara kubwa dhidi ya Kanali ya Suez. Sababu ya kufanywa mashambulio hayo ambayo baadaye yalikuja kujulikana kwa jina la Vita vya Kanali ya Suel, ni hatua ya Rais Gamal Abdul-Nassir wa Misri kuitangaza kanali hiyo kuwa mali ya taifa. Umoja wa Mataifa uliiunga mkono Misri wakati wa mashambulio hayo na kwa utaratibu huo tawala tatu hizo, yaani Uingereza, Ufaransa na utawala wa Kizayuni wa Israel zikaondoa majeshi yao katika ardhi ya nchi hiyo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!