Licha ya kuendelea kwa zoezi la kuhesabu kura nchini Madagascar,
wagombea wakuu wa nafasi ya urais wameanza kutuhumiana kwa uchakachuaji
wa kura nchini humo. Robinson Jean Louis anayeungwa mkono na Marc
Ravalomanana, Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyeng'olewa madarakani,
anamtuhumu mgombea mwenza Hery Rajaonarimampianina anayeungwa mkono na
Rais anayeondoka madarakani Andry Rajoelina, kwa kufanya njama za
uchakachuaji wa kura ili aibuke mshindi. Hii ni katika hali ambayo kwa
upande wake Hery naye amemtuhumu hasimu wake huyo kwa tuhuma hizo hizo.
Duru ya pili ya uchaguzi nchini Madagascar ilifanyika siku ya Ijumaa tarehe 20 za mwezi huu wa Disemba. Katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka huu, hakuna mgombea aliyeweza kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura suala lililopelekea kuitishwa duru ya pili ya uchaguzi huo. Duru za habari kutoka Antananarivo zinaripoti juu ya kuwepo mchuano mkali kati ya wagombea wawili wa uchaguzi huo ambao ni Robinson na Hery. Wananchi wanautaja uchaguzi huo kama hatua moja mbele katika kumaliza mgogoro wa kisiasa uliodumu kwa miaka kadhaa nchini Madagascar.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!