Kwa mara nyingine Rais Michel Djotodia wa jamhuri ya Afrika ya Kati,
ametaka kufanyika mazungumzo kati ya pande zinazogombana kwa ajili ya
kumaliza machafuko nchini humo. Djotodia ambaye pia ni kiongozi wa
zamani wa muungano wa waasi wa SELEKA na rais wa sasa wa serikali ya
mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati amesisitiza juu ya udharura wa
kufanyika mazungumzo kati ya pande hasimu na hivyo kuikwamua nchi hiyo
na hali ya mchafukoge inayoendelea hadi sasa. Aidha Rais Djotodia
ameyataka makundi yote ya wabeba silaha yakiwemo yale ya kidini kuweka
chini silaha zao na kufuata mkondo wa amani. Tangu mwanzoni mwa mwezi
huu wa Disemba, mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, umekuwa ukishuhudia
mapigano makali yaliyopelekea karibu watu 1000 kuuawa. Hayo yanajiri
katika hali ambayo ripoti kutoka mji mjini Bangui zinasema kuwa,
shughuli katika mji huo zimeanza kurejea katika hali ya kawaida baada ya
siku kadhaa za machafuko na mapigano yaliyozorotesha usalama na
shughuli mjini hapo.
Home »
siasa afrika
» RAIS MICHEL DJOTODIA AOMBA KUFANYIKA KWA MAZUNGUMZO CAR
RAIS MICHEL DJOTODIA AOMBA KUFANYIKA KWA MAZUNGUMZO CAR
Written By Unknown on Sunday, 22 December 2013 | Sunday, December 22, 2013
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!