KOCHA Mkuu wa Manchester United, David Moyes, amesisitiza kuwa
Robin van Persie na Shinji Kagawa si wachezaji walio kwenye orodha ya
watakaopigwa bei katika uhamisho utakaofanyika Januari mwakani.
Kocha huyo anataka kubaki na nyota wake wote
watano kwenye safu ya ushambuliaji ambao ni Van Persie, Wayne Rooney,
Danny Welbeck, Javier Hernandez na Kagawa.
Kwenye maelezo yake, amefuta pia mpango wa
kumsajili straika wa Monaco, Mcolombia Radamel Falcao na badala yake
anasaka viungo wawili makini wa kuimarisha timu hiyo yenye maskani yake
Old Trafford.
Baada ya kuwashuhudia mastraika wa wenzake
wakifanya vizuri kwenye timu zao, anaamini Van Persie atarejea uwanjani
kwa kasi na kuonyesha makali yake kama kawaida katika michuano hiyo.
Luis Suarez na Sergio Aguero wanatesa kwa sasa
kwenye ligi hiyo, huku straika wa Liverpool, Suarez, akiongoza kwa
ufungaji baada ya kutikisa nyavu mara 19 hadi kufikia sasa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!