ARSENAL imeshindwa kuiondoa Liverpool kileleni kwenye msimamo wa
Ligi Kuu ya England na hivyo kukubali kuuachia rasmi usukani baada ya
jana
Jumatatu usiku kushindwa kutamba mbele ya Chelsea baada ya kutoka sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Emirates.
Sare hiyo inaifanya Arsenal kufikisha pointi 36
sawa na Liverpool, lakini ikizidiwa kwa mabao na hivyo kuishia kushika
nafasi ya pili, lakini ikiwa
imepanda kwa nafasi moja baada ya wikiendi iliyopita kuporomoka hadi kwenye nafasi ya tatu kabla mechi yao hiyo.
Kitendo hicho pia kinaendelea rekodi mbovu ya
kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kushindwa kutamba mbele ya Jose
Mourinho, anayeinoa klabu ya Chelsea.
Arsenal iliyokuwa nyumbani ilihitaji kuibuka na
ushindi ili kurejea kwenye usukani wa ligi, lakini sasa matokeo hayo
wanawafanya kukaribisha Krismasi wakiachia uongozi wa ligi na kuifanya
Liverpool kutesa.
Kwa muda wote wa mchezo, timu hizo mbili zilicheza
kwa tahadhali kubwa na kushambuliana kwa zamu huku kipindi cha kwanza,
Chelsea ilionyesha kutaka ushindi baada ya mashambulizi makali ikiwamo
tukio la kugongesha mwamba baada ya shuti la Frank Lampard.
Kilio cha Mourinho dhidi ya mastraika wake kushindwa kufunga bao lolote ugenini kwenye ligi msimu huu kiliendelea baada ya straika pekee aliyepata nafasi ya kucheza, Fernando Torres kushindwa kuonyesha cheche zake kabla ya kutolewa na nafasi yake kuingizwa beki Mbrazili David Luiz.
Kilio cha Mourinho dhidi ya mastraika wake kushindwa kufunga bao lolote ugenini kwenye ligi msimu huu kiliendelea baada ya straika pekee aliyepata nafasi ya kucheza, Fernando Torres kushindwa kuonyesha cheche zake kabla ya kutolewa na nafasi yake kuingizwa beki Mbrazili David Luiz.
Kwenye kipindi cha pili, Arsenal walionekana
kusaka ushindi na kutengeneza nafasi kadhaa za mabao, lakini walishindwa
kuzitumia vizuri baada ya straika wake Olivier Giroud kukosa umakini.
Wakati Chelsea ikijivunia shambulizi la kugongesha
mwamba, Arsenal nao chupuchupu watikise nyavu baada ya beki wa Chelsea
kuokoa mpira kwenye mstari uliokuwa ukielekea wavuni na hivyo hadi
filimbi ya mwisho matokeo yalikuwa sare ya bila kufungana.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!