STRAIKA wa Liverpool, Luis Suarez, kwa sasa yupo kwenye
mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kubaki Anfield, lakini
Jumatatu iliyopita aliripotiwa kutoa mpya baada ya kukubali kusaini
mkataba feki wa miaka mitano ulioandaliwa na shabiki mmoja unaomtaka
endelee kuichezea timu hiyo.
Kwa mujibu wa 101greatgoals.com, staa huyo wa
kimataifa wa Uruguay, alikuwa akisaini vitabu na vitu mbalimbali vya
mashabiki wa Liverpool wakati alipokwenda kupokea tuzo yake ya
Shirikisho la Mashabiki wa Soka Jumatatu iliyopita.
Kwenye tukio hilo la kusaini vitu vya mashabiki,
straika huyo alisaini kipande cha karatasi kilichoandaliwa kama mkataba
kilichosomeka: “Nathibitisha kujitolea hatima yangu kwa miaka mitano
ijayo kwenye klabu ya soka ya Liverpool.”
Lakini, wakati mkataba huo ukiwa hauna maana
yoyote, staa huyo anayeongoza kwa mabao kwenye Ligi Kuu England msimu
huu hadi sasa, ameanza mazungumzo ya ujira mpya ndani ya timu hiyo huku
ripoti zikibainisha Liverpool imemwandalia ofa nono ya mshahara wa Pauni
200,000 kwa wiki.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!