Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar amesema kuwa, vikosi vyake
vimefanikiwa kuchukua udhibiti wa jimbo muhimu la uzalishaji mafuta la
Unity nchini humo. Makamu huyo wa zamani wa rais amedai kuwa, vikosi
vyake ambavyo vinapambana na askari wa serikali vinadhibiti sehemu kubwa
ya nchi hiyo. Kabla ya hapo pia jeshi la Sudan Kusini lilikuwa
limetangaza habari ya kujiengua serikalini jenerali JamesKwang Chol
aliyekuwa kiongozi wa kijeshi katika jimbo hilo la Unity nchini humo na
kujiunga na waasi. Wakati huo huo Umoja wa Afrika umetaka kurejeshwa
mara moja kwa usalama na amani nchini Sudan kusini, kufuatia mapigano
makali yanayoendelea nchini humo na kuwepo uwezekano wa kuzuka vita vya
ndani vya wenyewe kwa wenyewe. Habari kutoka Addis Ababa, Ethiopia
zinasema kuwa, ripoti iliyotolewa na Umoja huo, imelaani vikali mauaji
dhidi ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na raia wasio na
hatia, yaliyotekelezwa katika kambi moja ya Umoja wa Mataifa nchini
Sudan Kusini na kutaka kusitishwa haraka mapigano nchini humo. Mapigano
hayo yalizuka siku ya Jumapili iliyopita mjini Juba, ambao ni mji mkuu
wa Sudan Kusini na kuenea katika maeneo mengine ya nchi hiyo. Aidha
mapigano hayo yameyaingiza katika uhasama makabila mawili ya Nuer na
Dinka ambayo nayo yameanzisha mapigano baina yao.
Home »
siasa afrika
» KWA SASA TUMESHALITEKA JIMBO LA UNITY,NA AU YAJA JUU:Machar
KWA SASA TUMESHALITEKA JIMBO LA UNITY,NA AU YAJA JUU:Machar
Written By Unknown on Sunday, 22 December 2013 | Sunday, December 22, 2013
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!