JUVENTUS imetozwa faini ya Pauni 4,140 baada ya wanafunzi
waliokwenda kutazama mechi yao Jumapili iliyopita kuimba nyimbo za
kejeli kuhusu kipa wa timu pinzani.
Watoto hao 12, 200 waliokuwa wameketi nyuma ya
mabao katika mechi dhidi ya Udinese kwenye Serie A, pia wana kosa la
kuwa katika eneo hilo la uwanja ambalo lilipigwa marufuku kwa matukio ya
aina hiyo.
Lakini, watoto hao walikuwa wakitoa lugha za kejeli dhidi ya kipa wa Udinese, Zeljko Brkic kila alipokuwa akipiga mipira.
“Nilitaka kusema kitu baada ya mechi, lakini
ninachohofia nisije kuchochea matatizo zaidi,” alisema Kocha wa Udinese,
Francesco Guidolin.
“Kwa klabu kama Juventus mahali ambapo kila kitu
ni kizuri, mahali ambapo hata uwanja unakufanya usidhani kwamba upo
Italia, inakera sana kusikia kelele kama zile za kejeli dhidi ya kipa.”
Watoto hao ni kama wamerithi tabia za mashabiki wa Italia kuwakejeli makipa wa timu pinzani wanapopiga mipira.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!