GWIJI la Manchester United, Paul Scholes, amesema wanasoka
chipukizi nchini England wanaumizwa na wingi wa nyota wa kigeni kwenye
Ligi Kuu England.
Scholes ambaye aliibukia Old Trafford mwanzoni mwa
miaka ya tisini, anaamini wachezaji makinda wa taifa hilo hawapati
nafasi ya kuonyesha ubora wao tangu wakiwa watoto tofauti na ilivyokuwa
wakati wake kutokana na sasa klabu nyingi kusajili wachezaji wengi wa
kigeni.
“Wakati sisi tulipoibukia, karibu wote tulikuwa
wachezaji wa England. Kulikuwa na mmoja au wawili tu kutoka Ireland au
Wales,” alisema Scholes.
“Lakini kwa sasa kuna mataifa saba au nane ya
Ulaya wachezaji wake wanakuja na kuibukia kwenye shule za klabu hiyo,
ukiacha wale wanaosajiliwa. Hili haliwezi kuwasaidia wachezaji
Waingereza. Lazima kuwekwe sheria maalumu kwa sababu kama si sasa basi
baadaye kutakuwa na madhara makubwa.”
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!