Rubani wa ndege ya kampuni ya Msumbiji iliyoanguka nchini
Namibia mwezi uliopita aliiangusha makusudi, wataalam wa masuala ya anga
wamedai. Ndege hiyo TM470 iliondoka Maputo kwenda Angola tarehe 29
November, lakini ilianguka na kuua watu wote 33 waliokuwemo.
Chuo cha masuala ya anga nchini Msumbiji kimesema rubani huyo
aliiangusha ndege makusudi. Sababu za rubani huyo kufanya hivyo
hazijulikani na uchunguzi unaendelea. Ndege hiyo ya Mozambican Airlines
ilianguka kwenye hifadhi ya taifa ya Bwabwata nchini Namibia.
Inadaiwa kuwa rubani wa ndege Hermino dos Santos Fernandes, alijifungia kwenye ‘cockpit’ na hakumruhusu rubani mwenzie kuingia ndani kabla ya ndege hiyo kuanguka. Uchunguzi umeonesha kuwa Dos Santos Fernandes alibadilisha mara tatu kwa mkono altitude ya ndege hiyo kutoka meta 11,500 hadi meta 18.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!