Imembidi Usher Raymond aliyemtambulisha Justin Bieber kwenye
mkondo mkubwa wa muziki duniani, atumie muda wake kuongea na mwimbaji
huyo kiutu uzima kufuatia misala kadhaa inayomuandama iliyompelekea
kutupwa selo na baadaye kupandishwa kizimbani huko Miami.
Kwa mujibu wa TMZ, Usher alisafiri hadi Panama ambapo alikutana na Bieber na meneja wake, Scooter Braun na walifanya kikao cha pamoja.
Kikao hicho kilichofanyika ufukweni (Panama Beach Resort), kilihudhuriwa pia na rafiki wa utotoni wa Justin Bieber, Ryan Butler, na kuonesha uwepo wao katika eneo hilo walipost picha kadhaa kwenye Instagram wakiwa na shabiki wa Bieber (Belieber).
Picha moja inamuonesha JB akiwa na shabiki mmoja wa kike na nyingine inamuonesha Usher akiwa na shabiki huyo pia katika eneo hilohilo.
Hakuna aliyeyasikia mazungumzo yao na nia ya kukutana kwao, lakini kwa kuzingatia hatari ya kwenda jela inayomkabiri mwimbaji huyo toka Canada, ni dhahiri kwamba maongezi hayo yatakuwa na mlengo wa kutaka kumsaidia na kumuweka katika mstari ulionyooka.
Alhamisi ya wiki iliyopita, Justin Bieber alikamatwa na Polisi huko Miami na kutupwa selo kwa masaa kadhaa, na kisha kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuendesha akiwa amelewa, kuvuta bangi na kutumia leseni iliyopitwa na muda. Aliachiwa kwa dhamana baada ya kutoa kiasi cha $2,500.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!