Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » RAIS WA AFRICA YA KATI AANZA KUTUMIKIA VILE ALIVYO VIAHIDI WAKATI ANAAPISHWA

RAIS WA AFRICA YA KATI AANZA KUTUMIKIA VILE ALIVYO VIAHIDI WAKATI ANAAPISHWA

Written By Unknown on Monday, 27 January 2014 | Monday, January 27, 2014

Rais wa muda wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba-Panza ameanza mkakati wa kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo iliyokumbwa na mapigano ya ndani akishirikiana na Waziri Mkuu wa serikali yake Andre Nzapayeke.
Nzapayeke ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika amesema kuwa kipaumbele cha kwanza cha shughuli za serikali ni kukomesha mapigano na machafuko yaliyoikumba nchi hiyo. Ameongeza kuwa atazungumza na pande zote na kuunda timu itakayoshughulikia maslahi ya taifa.
Nzapayeke amesema kuwa serikali yake wiki hii itaanza kuchukua hatua za maana za kurejesha amani na utulivu na kuwarejesha wakimbizi katika makazi yao.
Matamshi hayo yametolewa huku ghasia na machafuko yakiendelea katika mji mkuu, Bangui hususan katika mitaa ya kibiashara yenye raia wengi Waislamu wanaoendelea kushambuliwa na wanamgambo wa Kikristo wa kundi la Anti Balaka.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi