Umoja wa Afrika umeitaka jamii ya kimataifa kuisaidia na kuiunga
mkono Madagascar baada ya kufanikiwa kutekeleza kwa njia ya kidemokrasia
zoezi la kukabidhiana madaraka. Baraza la Usalama la Amani la Umoja wa
Afrika limesisitiza kwamba, jamii ya kimataifa inapaswa kuiunga mkono
Madagascar ili kulinda kile kilichopatikana nchini humo baada ya
uchaguzi wa mwezi Disemba mwaka jana. Aidha Baraza la Amani la Usalama
la Umoja wa Afrika limemtaka Rais mpya wa Madagascar na mirengo mingine
ya kisiasa nchini humo kufanya juhudi za kuimarisha maridhiano ya
kitaifa na kuheshimu haki za binadamu.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Madagascar imerudishiwa uanachama wake katika Umoja wa Afrika baada ya nchi hiyo kuendesha uchaguzi wa Rais na Bunge uliokuwa huru na wa haki. Nchi hiyo ilivuliwa uanachama mwaka 2009 baada ya Andry Rajoelina kuchukua madaraka kwa uungaji na himaya ya jeshi. Mapinduzi hayo pia yalisababisha nchi za Ulaya kusimamisha misaada yao na hivyo kuyumbisha mno uchumi wa kisiwa hicho ambacho ni cha nne kwa ukubwa duniani.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!