Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , , » BIFU YA WALE WANAMUZIKI WAWILI MAARUFU KUTOKA NCHINI BURUNDI IMERUDI TENA KUFUFUKA UPYA

BIFU YA WALE WANAMUZIKI WAWILI MAARUFU KUTOKA NCHINI BURUNDI IMERUDI TENA KUFUFUKA UPYA

Written By Unknown on Tuesday, 21 January 2014 | Tuesday, January 21, 2014



Ukiuliza muziki wa kizazi kipya nchini Burundi lazima utawauulizia watu wa wili akiwemo huyu jama Niyonzima Salum Nassor ama Lolilo au Baba Rahma na mwenzie ajulikanae kama Mugani Desire.
Mu waanzilishi wa muziki huyu wa kizazi kipya huyu jama na Mugani Desire ama Big Fizzo ndio walio leta harakati kubwa na shambra shambra kwenye huyo muziki.Hapo mwanzo walipoanza kujenga jina wote wawili kwa kutaka kufahamika enzi hizo wakiimbia kwenye beat za magharibi mwa dunia walikuwa watu wakaribu sana huku istoshe wao ndo walikuwa kwenye chati za juu kwenye huyo muziki kipindi hicho.
Ila wawili hawa vile myaka ilivyokuwa inazidi kuongezeka na majina yao kuzidi kupanda nakuanza kukubalika walianza chuki za chini kwa chini huku kila raia akijiuliza chanzo cha chuki hiyo hakuna jibu.
Lolilo akiwa ndani ya Changamka show kwenye Rema fm
Ila kulikuwa na fununu kuwa chanzo nikuwa Lolilo pindi yuko nje ya nchi pande za ulaya aliwahi kupata taarifa zakuwa Farious ali copy na ku paste wimbo wake wa Baza.
Bifu hiyo ilikuwa imekaa kimya kwa muda mrefu uliyo pita ila kwa sasa imeonekana kupanda juu tena zaidi.
Chanzo cha bifu hiyo kufufuka hakijafahamika haswa huku fununu zikisema kuwa ni ile kauli ambayo Lolilo aliyo itamka kwenye kipindi cha Changamka Show kinacho endeshwa na Mtangazaji Mh Ismail Niyonkuru.
Kauli hiyo Lolilo aliitamka baada yakuilizwa na raia umoja aliye piga simu naku muuliza kuwa kwamba nikweli ayasemayo kuwa hana bifu na Fizzo?
Lolilo alijibu tena nakusema:"Sina bifu na Fizzo wala na Sony mimi nimtu wa Peace na nina mpango ikiwa Fizzo yuko tayari mi ntafanya nae ngoma akitoka nje"hayo Lolilo aliyasema pindi Fizzo hayupo hapa nchini alikuwa yupo Kigali Rwanda.

 

Inje mlangoni Kwa Vyisi
Baadhi ya raia walionekana kumpa sapoti Lolilo kwa kuonekana kujishusha nakuamuwa kutangaza kufanya colabo na huyo mpinzani wake.
Ila Farious madai hayo alipo tafutwa na mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru kutaka ajibu kuhusu swala hilo ila Star huyo wa Bajou alionekana kumkwepa mwanahabari huyo.
Ila moto umeonekana kurudi kururumba upya baada ya ya concert ya jumapili iliyo pita pande za kwa Vyisi Kanyosha kusini mwa mji Mkuu Bujumbura ambapo ilikuwa ni Show yakuwapambanisha wawili hao.
Wanamuziki Sat-b,Black-G na DJ Proo wakiwa ndani ya hilo gari wakiwasili kwenye show hiyo
Mapema zaidi wawili hao walikuwa walishatangaza kuwa watakuwepo wote wawili na bila yeyote kumuokopa mwenzie ila sharti wapewe malipo yao mapema.

 
 
Kwa upande wa Lolilo palionekana kuchelewesha malipo yake nakuamua kutangaza kuwa wamtowe kweny bango hilo na ilhali alikuwa aliwekwa bila taarifa zozote kutoka kwake.
Ila kutokana na mazungumzo mazuri Lolilo baadae alionekana kukubali kuwa atakuwepo kwenye mpambano huwo.
Watu kibao walionekana kuitikia tamasha huku wakitaka kushuhudia nani mkali au nani anaweza?
Kati ya hawo wawili palionekana vuta ni kuvute ya nani atakae anza kuimba.
Vuta ni kuvute hiyo ilimalizika na Fizzo kuamuwa kupanda kuanza yeye kuimba kwenye stage.
Siasa ya Fizzo hakuna alie kuwa anaitambuwa ila siasa ya Lolilo kila mtu alikuwa anaitambuwa kuwa ni ile ile tunayo izoweya yakutaka aimbe mwisho,Lolilo alitaka aimbe mwisho ili awe funga mlango yani mmaliziaji.
Ila Fizzo akaitumia vyema siasa yake yakupiga nyimbo zote na za uvunguni bila kuchoka huku muda ukizidi kurepa.
Kama vile unavyo fahamu fika Concert za Bujumbura ifikapo saa nne yani (22h) lazima kila bar au sehemu yote ya burudani ya wazi iwe imefungwa kwa sheria iliyo tolewa na serikali.
Fizzo akautumia muda huwo kwa kutwanga nyimbo zake zote hadi muda ambao yeye aliamuwa kushuka.
Inasemekana muda ambao aliwoshukia kulikuwa kumewadia muda wa kufunga bar hiyo ya kwa Vyisi na inasemekana walinda usalama walikuwa tayari walisha wasili kwenye uwanja wa bar hiyo wakisubiri amalize na wao wafanye kazi yao iliyo waleta.
Kabla ya hapo walinda usalama walikuwa wamezima kwa muda show hiyo ila baadae ikaendelea.
Lolilo alikuwa ameelekezwa na mpenzi wake Loliane
Lolilo akiondoka ndani ya gali lake
Lolilo ambae alikuwa amekania kivile huku akibadili fashion nakuweka mambo ya ninja yeye na ma dancer wake wote.
Ila ile siasa yake ilionekana kuingiliwa na giza pindi alipo panda kwa stage mataa yalizimishwa huku akisalia akihaha haha mbele ya macho ya raia wakimtazama akikosa lakufanya.
Lolilo aliamuwa kushuka kwa stage pindi alipo shuka inasemekana aliweza kupigwa chupa la beer la aina ya Heineken kwenye mkono wa kusoto.
Kitendo hicho kilimuuma roho sana kikachangia nakuzimiwa mataa na kuchomolewa speker asiimbe.
Hali hiyo ilionekana kupamba moto,huku asubuhi ya Jumatatu ilikuwa moto zaidi ambapo kila sikio la raia lilikuwa kwenye Radio Rema Fm wakisubiria nini Mtangazaji Mh Ismail Niyonkuru ataongea kwa yaliyo tokea jumapili kwenye show hiyo.
Kila raia alie kuwepo pale na wanamuziki walionekana kulaani kitendo hicho alicho tendewa Lolilo.
Hii leo tena kwenye kipindi cha Changamka show kinacho endeshwa na mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru alikuwa amewaalika wasanii hao wote wawili lakini umoja wao alishindwa kutokea kwenye kipindi.
Lolilo alionekana kuwa mwenye jazba alipo wasili tu kwenye studio nakuonekana kuwa mwenye uzuni nakumuona mtangazaji Mh Ismail Niyonkuru kama mokozi wake wakumpa nafasi yakutoleya yake yote ya moyoni.


Lolilo akilia kwenye kipindi
Lolilo alisisitiza nakusema kuwa kama Fizzo anataka bifu na yeye aanze yeye yupo tayari nakusema kuwa ameumizwa na kile kitendo alicho tendewa nakuonekana kuhadisia makosa yote aliyo tendewa na Fizzo pindi wangali marafiki.Akiendelea kuhadisia na kujibu ma swali ya raia kwenye kipindi Lolilo alionekana kuzidiwa na uchungu hadi kudondosha machozi........
Lolilo aliendelea kujibu majibu ya raia huku simu za pole zikikithiri kwenye kipindi.
Lolilo alionekana kulifasili jina la Farious nakusema maana yake ni mtu mwenye roho mbaya sana.
Karatasi ya makubaliano ya show
Hadi sasa hakuna anae fahamu ukweli uko wapi kati ya hao wawili huku Lolilo akimshtumu Fizzo kuwa yeye ndie alie cheza dili na walinda usalama kumzimia mataa na kuchomowa nyaya zote kutaka na yeye asiimbe akikifananisha kitendo hicho na kile kilicho tokea kwenye uwanja wa EPHU Nyakabiga pia akimshtumu kuwa yeye ndie alie cheza dili na ma Dj wamzimie mic namkumnyima mic mbili na wakati yeye alikuwa na mwenzake ila Fizzo alipo pand jukwani na rapa Uncle Crazy walipewa Mic mbili nakumalizia kuwa ni yeye alie cheza dili na watu walio husika nakuchomowa nyaya za umeme ili mwanamuziki Jaguar kutoka Kenya asiimbe na kweli Jaguar alisalia kupanda kwenye jukwaa kama Lolilo na kutoka bila kuimba.
Hiyi ndo karatasi ya makubaliano
Taarifa ambazo Lolilo aliacha Redioni nikuwa anataka kuwafungulia mashtaka wa andaaji wa show hiyo ambao walisema hawato mlipa pesa inayo salia baada yakupewa Advance huku na yeye akisema si mimi niliye kataa kuimba.
Lolilo akila pozi na Mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru



e kataa kuimba.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

1 comment:

  1. wewe ismail jichunge saana kwa maana unaweza kuwa chanzo cha bifu hizo....inaonekana wewe na fizzo hamuskilizani..kwanza kati ya hizi picka ulizo ziweka za fizzo ziko ngapi???mbona za lolo ndiyo nyingi???

    ReplyDelete

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi