STAA wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa, Franck
Ribery anaamini kuwa Cristiano Ronaldo hakustahili tuzo ya mwanasoka
bora wa dunia aliyopewa wiki iliyopita jijini Zurich.
Ronaldo alishinda tuzo hiyo mbele ya Lionel Messi
na Ribery mwenyewe, lakini Ribery anaamini kuwa mwanasoka huyo
hakustahili tuzo kwa sababu hakushinda taji lolote msimu uliopita.
“Nilishinda kila kitu na Bayern Munich pamoja na
mimi binafsi. Kwa upande mwingine Ronaldo hakushinda kitu chochote.
Sihuzuniki kwa kushindwa, lakini inauma kidogo. Nilistahili kutwaa
tuzo,” alisema Ribery.
“Ilikuwa wazi kwamba Ronaldo angeshinda. Upigwaji
wa kura uliongezewa muda kwa wiki mbili zaidi. Haijawahi kutokea hivi.
Haikuwa kuhusu soka tena, ulikuwa uamuzi wa kisiasa.” Aliongeza Mfaransa
huyo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!