KIUNGO wa Kibrazili, Ricardo Kaka amerudi kwenye ubora wake AC
Milan, lakini alipoulizwa mwenyewe akasema ana hasira na Kombe la Dunia.
Staa huyo alisema moja ya sababu kubwa
zilizomwondoa Real Madrid na kurejea AC Milan ni kupata nafasi ya
kuonyesha kiwango chake uwanjani ili kumshawishi kocha Luiz Felipe
Scolari amjumuishe kwenye kikosi chake kwa ajili ya fainali zijazo za
Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil kati ya Juni na Julai mwaka huu.
Alipozungumza na Globo TV, Kaka alisema dhamira
kubwa ya kiwango chake ni kucheza Kombe la Dunia na hilo ndilo
lililomfanya ang’oke Santiago Bernabeu na kurejea San Siro kwenye majira
ya kiangazi mwaka jana.
“Natumai kuwapo kwenye kikosi cha mwisho. Sifahamu
itakavyokuwa, kwa sababu mambo yanakuwa magumu sana. Kombe la Mabara
liliisaidia Brazil kupata kundi fulani la wachezaji,” alisema staa huyo
wa Rossoneri.
Kaka bado anaishi kwa kumbukumbu ya maneno ya
Scolari kwamba atamrudisha kikosini Brazil kama ataboresha kiwango chake
na kucheza kwa daraja la juu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!