André Nzapayeke, Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
ametangaza baraza jipya la mawaziri la serikali ya muda ya nchi hiyo
iliyokumbwa na machafuko. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
amewabakisha mawaziri wengi waliokuweko katika serikali iliyopita ya
Rais Michel Djotodia. Aidha katika baraza hilo jipya la mawaziri, Waziri
Mkuu Andre Nzapayeke amemteua waziri mmoja kutoka katika kundi la waasi
wa Kikristo wa Anti-Balaka wanaoendesha mauaji dhidi ya Waislamu wa
nchi hiyo.
Serikali hiyo inaundwa na mawaziri 20. Aidha wanawake saba ni miongoni mwa mawaziri wanaounda baraza hilo jipya la mawaziri ambalo linakabiliwa na changamoto kubwa ya kurejesha amani na uthabiti nchini humo. Mawaziri wawili wa Wizara ya Huduma za Jamii na ile ya Ujenzi wa Miji wanaohesabiwa kuwa watu wa karibu wa Michel Djotodia aliyelazimika kujiuzulu kutokana na mashinikizo ni miongoni mwa mawaziri waliobakishwa katika baraza hilo jipya la mawaziri.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!