MSHAMBULIAJI wa klabu ya
Liverpool, Luis Suarez ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Desemba wa
Ligi Kuu nchini Uingereza huku meneja wa Manchester City Manuel
Pellegrini akitajwa kama kocha bora wa mwezi. Suarez ambaye anakipiga
katika klabu ya Liverpool alianza mwezi vibaya baada ya timu hiyo
kukubali vipigo kutoka kwa Hull City, Manchester City na Chelsea lakini
alionyesha kiwango cha juu baadae kwa kufunga mabao 10 katika mechi nne
pekee.
Mabao hayo alifunga
katika mechi dhidi ya Norwich City ambapo alifunga manne, West Ham
United mabao mawili, Totehham Hotaspurs mabao mawili na mengine mawili
katika mchezo dhidi ya Cardiff City. Mabao hayo yaliisaidia Liverpool
kushika usukani wa ligi katika kipindi cha Christmas iangwa baadae
waliteleza mpaka nafasi ya tano katika kipindi cha mwaka mpya. Naye
Pellegrini mwezi Desemba ulikuwa mzuri kwake baada ya kushinda mechi
zote sita kati ya saba walizocheza huku mmoja wakitoka sare ya kufungana
bao 1-1 na Southampton.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!