Umoja wa Mataifa umesema kuwa
unatiwa wasiwasi na ukosefu wa usalama wa chakula nchini Somalia.
Kitengo cha kuchunguza usalama wa chakula na lishe cha Umoja wa Mataifa
kimesema kuwa, uhaba wa mvua, mafuriko na tufani haribifu ndio sababu
muhimu iliyopelekea ukosefu wa mazao katika eneo la Puntland kaskazini
mashariki mwa Somalia. Naye Naibu Mkuu wa Hospitali ya Banadir mjini
Mogadishu amesema, mafuriko yaliyotokea kusini mwa nchi hiyo na majanga
mengine ya kibinadamu yameathiri uzalishaji wa chakula nchini humo.
Inakadiriwa kuwa, watu wasiopungua laki 8 na 80 elfu ambao wengi wao
wamekimbia makaazi yao nchini Somalia bado wanahitajia misaada ya haraka
ya kibinadamu.
Pia zaidi ya Wasomali milioni 2 wanaishi bila kuwa na chakula cha kutosha.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!