Siku kama ya leo miaka 35
iliyopita gwaride la mwisho na kimaonyesho la vikosi vya majeshi ya
utawala wa Shah lililokuwa na lengo la kuwatia hofu na woga wananchi
Waislamu wa Iran, lilifanyika katika mitaa mbalimbali ya Tehran. Katika
gwaride hilo, wanajeshi wengi walionesha mshikamano wao na kuungana na
wananchi Waislamu wa Iran na kuamua kuanza mapambano dhidi ya utawala wa
kibeberu wa Shah.
Miaka 164 iliyopita katika
siku kama hii ya leo ilianza harakati kubwa ya wananchi wa China
iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Taiping, yenye maana ya 'Irada ya
Watu'. Harakati hiyo ilitokana na hali mbaya na umasikini uliokuwa
ukiwasumbua wananchi wa nchi hiyo na hasa matabaka ya vijijini,
iliyosababishwa na ukoloni wa kigeni na utawala wa familia isiyofaa ya
Manchu. Lengo kuu la harakati hiyo iliyoendelea kwa muda wa miaka 14
lilikuwa kuanzisha usawa katika kugawana ardhi kati ya wanawake na
wanaume.
Na siku kama ya leo miaka 415
iliyopita, ilianzishwa kampuni ya Kiingereza ya India Mashariki nchini
India, kwa amri ya Malkia Elizabeth wa Kwanza wa Uingereza. Baada ya
Uingereza kujikita nchini India, nchi kama vile Uholanzi, Ureno na
Ufaransa zilielekea upande wa Bara Hindi kwa lengo la kutafuta makoloni
mapya. Baada ya karne 3 tangu kuanzishwa shirika hilo, satuwa na
kuimarika utawala wa Uingereza nchini India vilisababisha nchi hiyo
kutangazwa kuwa sehemu ya Uingereza na kuvikwa taji Malkia Viktoria kama
mtawala wa India na Uingereza. Katika kipindi hicho rasilimali nyingi
za India ziliporwa na serikali na mabeberu wa Uingereza.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!