Shirika la kutetea haki za binadamu
la Human Rights Watch limetaka ukatili uliofanywa katika vita vya Sudan
Kusini uchunguzwe kikamilifu, likiripoti kuwa katika mji mmoja pekee
kumepatikana miili iliyochomwa moto na makaburi ya umati. Skye Wheeler
msemaji wa HRW amesema, jinai za kutisha zimefanyika kwenye mji huo na
maeneo mengine ya Sudan Kusini ukiwemo mji mkuu Juba, ambapo watu wengi
waliuawa kikatili kutoka makabila yote hasimu. Shirika hilo la kutetea
haki za binadamu limesisitiza kuwa, kufikishwa wahusika katika vyombo
vya sheria ni jambo muhimu ili kusonga mbele na kuzuia kurudiwa
machafuko nchini humo.
Inakadiriwa kuwa mapigano ya Sudan
Kusini kati ya vikosi vya serikali na waasi yamepelekea maelfu ya watu
kuuawa na wengine laki 8 kukimbia makaazi yao.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!