BEKI wa West Ham,Guy Demel alilazimika kuwahishwa hospitalini
baada ya kupata majeraha ya kichwa kwenye mechi ya Ligi Kuu England
dhidi ya Cardiff City juzi Jumamosi.
Demel, 32, alilazimika kupumua kwa mtambo wa gesi
wakati alipokuwa akitolewa uwanjani kwa machela alipoanguka na kupoteza
fahamu baada ya kugongana na straika wa Cardiff City, Fraizer Campbell.
“Demel alizimia na alikuwa kwenye hali mbaya kwa
dakika kadhaa. Hivyo alibaki hospitali kwa huduma zaidi,” aliandika
mmiliki wa West Ham United, David Gold kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Kuumia kwa beki huyo kunamfanya kuungana na mabeki wa wengine wa kikosi hicho ambao ni wagonjwa: Winston Reid na James Collins.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!