BAADA ya vita vya maneno
vya kipidi kirefu juu ya mchezaji gani haswa anastahili tuzo ya
mchezaji bora duniani wa mwaka 2013 inayojulikana kama Ballon d’Or
hatimaye kitendawili hicho kinaratajiwa kuteguliwa baadae leo katika
sherehe za utoaji tuzo hiyo zitakazofanyika jijini Zurich,
Switzerland. Nyota watatu walioteuliwa katika orodha ya mwisho ya
kugombea tuzo hiyo ni nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo anayecheza klabu
ya Real Madrid, Muargentina Lionel Messi anayecheza Barcelona na
Mfaransa Franck Ribery anayecheza Bayern Munich. Safari hii mpambano
unaonekana kuwa mkali kati ya Ribery na Ronaldo ambao wamekuwa katika
kiwango bora huku kila mmoja akiisaidia klabu na timu yake ya taifa
kufikia mafanikio waliyopata mwaka jana. Messi ambaye anashikilia tuzo
hiyo kwa miaka minne mfululizo anaonekana kutokuwa na nafasi ya kutosha
kulinganisha na wenzake baada ya kuanza msimu vibaya kwa kuandamwa na
majeruhi ya mara kwa mara ambayo yamepelekea kumuweka nje ya uwanja kwa
karibu miezi miwili. Kila mtu amekuwa na maoni tofauti kuhusiana na
wachezaji hao na viwango vyao walivyoonyesha mwaka jana lakini waamuzi
wa mwisho watakuwa ni makocha na manahodha wa timu mbalimbali za taifa
duniani ambao ndio waliokuwa wakipiga kura kuchagua mmoja wapo.
Home »
michezo ulaya
» MESSI,RONALDO NA RIBERY NANI AMBAE LEO ATANYAKUWA MPIRA WA DHAHABU?
MESSI,RONALDO NA RIBERY NANI AMBAE LEO ATANYAKUWA MPIRA WA DHAHABU?
Written By Unknown on Monday, 13 January 2014 | Monday, January 13, 2014
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!