Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » IMEGUNDULIKA KUWA JUSTIN BIEBBER ANATUMIA MADAWA YAKULEVYA AMBAYO YANAWEZA KUMUONDOWA DUNIANI

IMEGUNDULIKA KUWA JUSTIN BIEBBER ANATUMIA MADAWA YAKULEVYA AMBAYO YANAWEZA KUMUONDOWA DUNIANI

Written By Unknown on Monday, 20 January 2014 | Monday, January 20, 2014

Justin Bieber ameingia kwenye orodha ya wasanii wakubwa wanaoishi katika hatari kubwa waliyoitengeneza wenyewe ambayo inaweza kuchukua maisha yao muda wowote.  
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kilichoongea na TMZ, mwimbaji huyo wa ‘As Long as You Love Me’ amekuwa akifanya mchanganyiko wa codeine, promethazine, Jolly Rancher na soda aina ya Sprite, mchanganyiko ambao unatengeneza ‘Sizzurp’ ambacho ni kilevi kinachoweza kuyachukua maisha yake wakati wowote ama kumsababishia kifafa.
Mwaka jana member wa Young Money, Lil Wayne alilazwa hospitali mara kadhaa akiwa hoi akisumbuliwa na kifafa na iliripotiwa kuwa alikuwa akitumia ‘Sizzurp’ kama afanyavyo J.B.
Hata hivyo ripoti zilizotelewa na chanzo hicho zinadai kuwa Bieber amekuwa akitumia Sizzurp mara kwa mara lakini kwa tahadhari kubwa.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 19, ameripotiwa kuwa huwa anatumia pia vidonge kama Xanax na kujipigilia pombe na marijuana, lakini hajawahi kabisa kutumia cocaine.
January 14, polisi walifanya upekuzi kwenye nyumba ya Bieber kufuatia tuhuma za kurusha mayai kadhaa kwa jirani yake ambapo walikuta dawa za kulevya aina ya cocaine na kumshikiria rafiki yake Lil Za aliyekuwepo nyumbani kwa Bieber siku hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi