Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » KAMA ULIKUWA HAUFAHAM HIVI NDO VILE USHINDI WA BURUNDI DHIDI YA MAURITANIA ULIVYO TAFUTWA MPAKA UKAPATIKANA

KAMA ULIKUWA HAUFAHAM HIVI NDO VILE USHINDI WA BURUNDI DHIDI YA MAURITANIA ULIVYO TAFUTWA MPAKA UKAPATIKANA

Written By Unknown on Monday, 20 January 2014 | Monday, January 20, 2014

Baada yakuzungumzwa mengi kuhusu timu ya Taifa ya Burundi ya Intamba mu Rugamba kuwekwa kwenye kundi D na timu kama GABON,MAURITANIA na DRC huku ukizisikia timu hizo ki majina unaweza kuziokopa ukifata na historia ambazo zinazo kwenye soka barani Africa.
Timu ya taifa ya Burundi ya Intamba mu Rugamba ilikuwa kwenye hali ngumu ya maandalizi ikiwemo na  ukosefu wa huduma tafauti kwa timu hiyo huku kukianza kuzungumzwa mengi kuwa timu hiyo haiwezi kufanya vyema kutokana kwa kukosekana kwa maandalizi yakutosha yakuelekea kwenye hiyo michuano yani maandalizi madogo huku wakiipimanisha na Timu kama DRC ambayo kikosi kizima kilifa mapema nchini Africa ya kusini ikiwa ni moja ya njia yakutaka wazowee hali ya hewa na kujipima nguvu na vilabu tafauti vya huko.

Timu ya taifa ya Burundi INTAMBA MU RUGAMBA imeanza kuonesha picha nzuri kwenye michuano ya CHAN 2014 huku ikianza kuwaacha midomo wazi wale wote ambao walikuwa wakihisi timu hiyi itaelekea huko kuoga ma bao,
hayo yote yameanza kubadilika nakuanza kuleta mtazamo mwingine.Kwenye match ya kwanza ya Burundi(INTAMBA MU RUGAMBA)dhidi ya Gabon haikuwa rais kwa timu hiyo ya Gabon yenye historia kubwa kwenye soka barani Africa ambapo Burundi ilicheza dakika 90' na ikailazimisha Gabon kutoka sare ya bila bila.
Baada yakutoka sare na Gabon,Burundi (Intamba Mu Rugamba) ilianza kuzungumzwa sana na vyombo vya habari barani Africa na dunia nzima kuwa ni timu yenye kutiliwa matumaini kama wataendelea na mchezo walio uonesha.
Warundi wengi wanao ifahamu vyema timu ya taifa ya Burundi ya Intamba mu Rugamba walionekana kuulani mfumo wa Coach Muhamed Lodfi mwenye asili ya Misri kwa kushindwa kuwapanga vyema wachezaji uwanjani.
Match ya pili kwenye kundi hilo D Burundi ilikutana na Mauritania ilikuwa Jumamosi usiku kwenye mida ya saa mbili usiku (20h00) majira ya Bujumbura.
Intamba ilijikita uwanjani baada ya Gabon kuibamiza DRC bao moja kwa nunge tena bao lenyewe la mapema kabisa ilikuwa kwenye mida ya saa kumi na moja za magharibi(17h00).
Intamba iliingia uwanjani ikiwa na vigogo wake 11 ikiwemo nahoza mkongwe Yamin Seleman na goal kipa wao mahiri Arakaza Mac Arthur.
Kwenye dakika sifuri ya mwanzo Intamba ilionekana kuzubalia mataa ya Africa ya kusini na zile screen kubwa za uwanjani walijikuta wakilambwa bao.
Match iliendelea huku kitumaini cha Intamba kusonga mbele siku hiyo kikaanza kukatika.
Baadhi ya wapenzi wa timu ya taifa walianza kutowa kitumaini cha timu hiyo kufika mbali.
Kwenye hicho hicho kipindi cha kwanza Intamba ilionekana kushamiri zaidi na kulishambulia lango la Mauritania kwa kiasi kikubwa.
Kwenye dakika ya 11 ya hicho kipindi cha kwanza kulipigwa mchongo mzuri kutoka kwa Nahodha wa timu ya Taifa Yamin Seleman hadi kwenye kichwa cha mkali Abdul Razaq Fiston hadi mpira wavuniii.
Kwenye hicho hicho kipindi cha kwanza Burundi ilipata pena baada ya mchezaji Claude alimaarufu kama Lambalamba kuangushwa kwenye eneo la hatari la Mauritania.
Hapo Mauritania ilianza kuona kuelemewa zaidi,pena hiyo ambayo ilipewa nahodha Yamin Selaman ila alioneka kushindwa kufanya vyema akisalia kuimpa goli kipa.
Walienda mapumziko wako moja moja,kwenye kipindi cha pili Intamba ilipigwa bao la pili kwenye mazingira yakusubiria kuwa mchezaji kaotea na kumbe sivyo na akauchapika wavuni ikawa mbili kwa moja huku mbili za Mauritania moja ya Burundi,kwenye dakika ya 61 mchezaji Nduwarugira Fiston aliweza kusawazisha bao hilo nakuifanya Burundi iwe sawa sawa na Mauritania.
match iliendelea hivo huku cha huku akiendi huku hadi kwenye dakika ya 90' wakiwa sawa sawa wote,ilibidi waongeze dakika 4' kwenye zile dakika 4' zanyongeza,mwishoni mwishoni mwa dakika hizo kukiwa kunasalia kama sekunde 15 hivo nahodha yamini Selemani aliweza kuifanya Intamba kufika kileleni baada yakupiga bonge la shuti ambalo kipa wa Mauritania aliona upepo akishtuka wavu ukitikisika.
Goaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaal...........................Yamin Seleman................


Kwa sasa Burundi inaongoza kwenye kundi D ikiwa mbele ya timu kama Gabon,Mauritania na Drc.
Burundi na timu zote hizo zinasalia na match moja moja huku match ya mwisho ya Burundi itapambana dhidi ya nchi jirani ya DRC itakayo chezwa hiyo Jumatano usiku kwenye  mida ya saa moja kamili yani (19h) ma saa ya Bujumbura.
Huku Burundi inaombwa vitu viwili kugawa au kufunga.

Mtandao wenu wa www.ismailniyonkuru.info unaitakia timu ya taifa ushindi nakuzidi kusonga mbele




TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi