Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa jana alilituhumu jeshi na
waasi wa Sudan Kusini wanaoongozwa na Riek Machar, Makamu wa zamani wa
Rais wa nchi hiyo kuwa wanaiba misaada ya chakula na magari yanayotumika
kusambazia chakula huku nchi hiyo ikikaribia kukumbwa na vita vya
wenyewe kwa wenyewe. Ofisi ya habari ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa
Ban Ki-moon anatiwa wasiwasi na kuongezeka idadi ya wahanga kutokana na
kuendelea mapigano huko Sudan Kusini, kukiwemo ripoti waliyoipokea jana
Januari 14 kuhusu vifo vya watu 300 waliozama katika ziwa Nile wakati
wakikimbia mapigano katika mji wa Malakal. Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa amelaani vikali hatua ya vikosi vya jeshi la Sudan Kusini na
waasi wa nchi hiyo ya kuiba magari, misaada ya chakula, na suhula
nyingine za kibinadamu.
Home »
siasa afrika
» "JESHI NA WAASI NCHINI SUDAN KUSINI WANAIBA MISAADA":UN
"JESHI NA WAASI NCHINI SUDAN KUSINI WANAIBA MISAADA":UN
Written By Unknown on Wednesday, 15 January 2014 | Wednesday, January 15, 2014
Labels:
siasa afrika
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!