Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita
kulitokea mapigano makali baina ya askari wa utawala wa Shah wa Iran na
wananchi baada ya maandamano ya mara kwa mara ya wananchi wa Iran dhidi
ya utawala wa kidikteta hapa nchini. Wakati huo baadhi ya wanajeshi wa
Shah ambao walielewa haki ya mapambano ya taifa la Iran walikimbia kambi
zao za kijeshi na kujiunga na wananchi. Hatua hiyo ilikuwa bishara
njema ya mageuzi ya kimsingi katika muundo wa jeshi la Shah. Wakati huo
kiongozi wa harakati za mapinduzi Imam Ruhullah Khomeini alitoa ujumbe
akihamasisha jeshi kujiunga na mapambano ya wananchi dhidi ya utawala wa
kidikteta wa Shah na kutetea Uislamu na sheria zake.
Tarehe 15 Januari miaka 175 iliyopita,
nchi ya El Salvador ilijitangazia rasmi uhuru baada ya kusambaratika
Muungano wa Amerika ya Kati. Hata hivyo nchi hiyo haikupata amani na
utulivu hata baada ya kupita karne moja. El Salvador ambayo ilikuwa
ikikoloniwa na Uhispania kwa miaka kadhaa, ilijipatia uhuru mwaka 1821,
na ulipofika mwaka 1824 ilijiunga na Muungano wa Amerika ya Kati, na
hatimaye uliposambaratika muungano huo, nchi hiyo ilijitegemea
kikamilifu.
Na siku kama ya leo miaka 1145 alizaliwa
Qadhi Jorjani maarufu kwa lakabu ya Abulhassan, faqihi, mwandishi na
malenga wa Kiislamu. Jorjani alifunzwa masomo hayo ya kidini na Qadhi
Mkuu wa mji wa Rei ulioko karibu na Tehran ya leo. Qadhi ameandika
vitabu vingi vya kielimu na miongoni mwake ni vile vya "Tafsirul Qur'an"
na "Tahdhib al Tarikh". Qadhi Jorjani alifariki dunia mwaka 366 Hijria
huko Neishabur na akazikwa huko Jorjan au Gorgan ya leo kaskazini
mashariki mwa Iran.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!