Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » JE,ULIKUWA UNA YAFAHAMU HAYA?BASI SOMA HAYA YALIYO PITA MYAKA KADHAA YANAYO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO YANI HISTORIA

JE,ULIKUWA UNA YAFAHAMU HAYA?BASI SOMA HAYA YALIYO PITA MYAKA KADHAA YANAYO AMBATANA NA SIKU KAMA YA LEO YANI HISTORIA

Written By Unknown on Sunday, 26 January 2014 | Sunday, January 26, 2014

Siku kama ya leo miaka 64 iliyopita na kufuatia  kutangazwa uhuru kutoka katika makucha ya mkoloni Mwingereza mwezi Agosti mwaka 1947 Miladia, mfumo wa jamhuri uliasisiwa huko India na Rais wa nchi hiyo akawa Dakta Rajendra Prasad ambaye aliliiongoza taifa kwa muda wa miaka saba.  Hata hivyo kwa mujibu wa mfumo wa India, wadhifa wa urais ni wa kiheshima tu, isipokuwa Waziri Mkuu ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za serikali.

Siku kama ya leo miaka 190 iliyopita, alizaliwa William Thomson anayefahamika kwa jina maarufu la "Lord Kelvin" mwanahisabati na mwanafizikia wa Ireland. Lord Kelvin alifanya utafiti wa kina kuhusu nishati ya joto na umeme katika sayansi ya fikizikia katika zama zake. Mwanzoni mwa utafiti wake huo, Kelvin aliweza pia kugundua teknolojia ya kutuma ujumbe kwa kutumia njia ya majini na kufanikiwa kutengeneza telegrafu inayopitia baharini. Mwanafizikia huyo alivumbua pia kifaa cha kutambua mawimbi na kupimia nguvu ya umeme au Galvanometer ambacho kilipewa jina la msomi huyo.

Siku kama ya leo miaka 36 iliyopita, mkataba wa Camp David ulitiwa saini katika eneo linalojulikana kwa jina hilo huko nchini Marekani kati ya Anwar Saadat Rais wa wakati huo wa Misri na Menakhim Begin Waziri Mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni kwa kuhudhuriwa na Jimmy Carter Rais wa wakati huo wa Marekani. Marekani ndiyo iliyoandaa mpango wa kusainiwa mkataba huo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, utawala wa Kizayuni ulirejesha udhibiti wa Peninsula ya Sinai au jangwa la Sinai kwa Misri na mkabala wake serikali ya Misri ikautambua rasmi utawala huo bandia.

Na miaka 191 iliyopita, yaani mwaka 1749 alifariki dunia Edward Jenner tabibu wa Kiingereza aliyegundua chanjo ya ndui yaani (small pox). Jenner alizaliwa mwaka 1749 Miladia. Tabibu huyo alifanikiwa kugundua chanjo ya ndui akiwa na umri wa miaka 45 wakati alipoelekea nchini India. Kuanzia hapo ugonjwa huo wa ndui uliweza kutibiwa kwa kutumia chanjo hiyo. Na ilipofika mwaka 1979 maradhi hayo yaliweza kutokomezwa kabisa duniani.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi