SIJUI ni hasira au nini! Mama mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu,
Mariam Sepetu ‘Mama Wema’ amemshika uchawi mpenzi wa bintiye, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ huku akilaani vikali kitendo cha kumrudia mwanaye akidai
lengo lake ni kumharibia maisha.
ALIANZAJE?
Mwanamke huyo mwenye msimamo uliopitiliza kuhusu bintiye Wema, aliwasiliana alisema kuwa siku hiyo anataka kutoa dukuduku lake kuhusu Diamond ambaye pia ni staa wa Bongo Fleva.
Mama Wema alisema taarifa alizonazo kuhusu staa huyo ni kwamba, juzikati alikwenda kwa mganga f’lani na kuzika kondoo watatu ili Wema aharibikiwe maisha.
“Mimi nimekerwa sana na huyo Diamond wenu. Najua hajamrudia Wema kwa mapenzi, amemrudia ili apate nafasi ya kumharibia maisha. Ni kijana hatari sana.
“Nina taarifa kutoka kwa watu wa karibu naye kwamba alikwenda kwa mganga akazika kondoo watatu ili mwanangu aharibikiwe.
“Simpendi na sitaki hata kumwona. Hana nia nzuri na mwanangu, najua. Kwanza mama Diamond (Sanura Kasim) hampendi Wema, anampenda Penny, nampongeza sana kwa uamuzi huo,” alisema mwanamke huyo.
AMSHANGAA DIAMOND KULALIA KITANDA CHA KIGOGO WA IKULU
Mama Wema ambaye anasifika kwa ubabe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa amesikia Diamond sasa analala na kula kwa Wema. Akatolea tamko kitendo hicho.
“Kama angekuwa mwanaume kweli ana pesa zake angekubali vipi kulala kwenye kitanda alichonunua mwanaume mwenzake (Clement)?
“Hiyo ni akili kweli? Vitu anunue mwanaume mwenzako halafu wewe uje kutumia bila haya. Halafu nimesoma kwenye gazeti moja eti atamnunulia Wema vitu vyote alivyonyang’anywa na Clement, mimi nasema hawezi kumnunulia kamwe, anamdanganya tu,” alisema mama Wema.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!