Licha ya
kuanza kurejea kwa hali ya utulivu kwenye baadhi ya maeneo nchini
Jamhuri ya Afrika ya kat,ila bado kumeripotiwa vurugu na mauaji ya wenyewe
kwa wenyewe kwenye miji mingi ambayo inakaliwa na wakristo. Vikosi vya
kulinda amani vya Umoja wa Afrika MISCA vimekuwa na kazi ya ziada
kuyadhibiti baadhi ya makundi ya vijana wa Kikristo kaskazini mwa nchi
hiyo kwenye mji wa Boali ambao wamekuwa wakitekeleza mauji dhidi ya
waumini wa dini ya kiislamu kwa madai ya ulipizaji kisasi dhidi ya ndugu
zao waliouawa.
Mkuu wa operesheni za kijeshi za majeshi ya MISCA nchini humo, Jenerali,
Jean Marie Michel Mukoko anasema kuwa kwa sasa wanalenga kuhakikisha
usalama mjini Bangui kabla ya kuelekeza nguvu zaidi kwenye maeneo ya
kaskazini mwa nchi hiyo ambako kuna mapigano yanaripotiwa.
Katika hatua nyingine bunge la mpito nchini humo leo hii linatarajiwa kupigia kura majina 8 yaliyowasilishwa bungeni na hatimaye kupata jina moja la kiongozi ambaye atakuwa rais wa mpito.
Hata hivyo bado kunashuhudiwa mgawanyiko mkubwa ndani ya kundi la waasi wa Seleka waliohusika kufanya mapinduzi nchini humo.
Umoja wa mataifa umeonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa mauji ya ulipizaji kisasi nchini humo dhidi ya waumini wa dini ya kiislamu.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!