DILI la kubadilisha wachezaji Wayne Rooney wa Manchester United
na Juan Mata wa Chelsea linaonekana bado lipo baada ya kubainika kuwa
Man United imetoa ofa ya kutaka kumchukua Mata katika dirisha hili la
Januari.
Inadaiwa kuwa kocha David Moyes anamtaka Mata
katika dirisha hili la Januari, huku kocha wa Chelsea, Jose Mourinho
akiwa anaeleweka kwa tamaa yake ya kutaka kumnasa Rooney kwa muda mrefu
sasa.
Hata hivyo inadaiwa kuwa Chelsea wanaweza
kumchukua Rooney katika dirisha la Januari na si wakati huu ambapo Man
United inamtegemea sana katika mbio za kusaka kuingia Top Four.
Mourinho yuko tayari kuongeza kiasi cha Pauni 20
milioni katika uhamisho huo kwa ajili ya kumpata Rooney, licha ya ukweli
kwamba staa huyo atakuwa amebakiza miezi 12 tu kumaliza mkataba wake
Old Trafford.
Wakati Mata akiwa ameruhusiwa kuondoka Stamford
Bridge baada ya kudorora kwa uhusiano wake na Mourinho, Rooney amegoma
kusaini mkataba mpya Man United huku yeye na wawakilishi wake
wakifikiria kuwa muda wa mchezaji huyo kuwa Old Trafford umepita.
Habari za ndani zinadai kwamba Mourinho pamoja na
kutokuwa tayari kuona Mata akikipiga katika klabu za England lakini
huenda akawa tayari na kulegeza msimamo wake huo kama suala la kumpata
Rooney linaweza kufanikiwa.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!