KOCHA, Jose Mourinho ametoa kali baada ya kubeba chupa yake ya
mvinyo na kisha kwenda nayo kwenye mkutano wa waandishi wa habari juzi
Jumanne ili kusherehekea miaka 51 ya kuzaliwa kwake.
Kocha huyo wa Chelsea alitaka kufurahia siku hiyo
muhimu kwake na waandishi wa habari na hivyo kuamua kubeba chupa nzima
ya mvinyo na bilauri kisha kwenda nazo kwa waandishi.
Kocha huyo alisema wiki iliyopita kwamba atakwenda
kuzungumza na waandishi wa habari akiwa na mvinyo wakati wa mazungumzo
ya kuhusu mchezo wao wa jana Jumatano dhidi ya West Ham United kwenye
Ligi Kuu England.
“Tutakunywa mvinyo pamoja kwa sababu tumebadilika sana. Naamini tutakunywa tena mvinyo huu hapo baadaye,” alisema Mourinho.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!