POLISI wa Merseyside, Liverpool wamethibitisha kwamba wanafanya
uchunguzi kumpata mtu aliyemrushia sarafu straika, Luis Suarez wakati wa
mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika Anfield juzi Jumanne usiku.
Liverpool ilimenyana na Everton katika mchezo wa mahasimu wakubwa Ligi Kuu England na wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Staa wa Liverpool, Suarez alidaiwa kulengwa kwenye
shambulio lililofanywa na mashabiki wa Everton wakati alipokwenda
kupiga kona ndipo aliporushiwa sarafu ambayo baadaye alimpata mwamuzi
Martin Atkinson.
Taarifa ya polisi kutoka Merseyside ilibainisha:
“Tunaweza kuthibitisha kwa sasa tunafanya uchunguzi kupata mtu
aliyehusika na tukio hilo. Tukio lenyewe lilitokea kipindi cha kwanza
baada ya sarafu kurushwa uwanjani na vitu vingine vyenye kuumiza.
“Maofisa wa polisi watatumia kamera za CCTV za uwanjani hapo kumpata mhusika au wahusika waliotenda tukio hilo.”
Kwenye mchezo huo, mabao ya Liverpool yalifungwa na Suarez, Steven Gerrard na Daniel Sturridge, aliyefunga mara mbili.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!