Miaka 45 iliyopita, siku kama ya leo,
alifariki dunia nchini Iraq Ayatullah Sayyid Muhsin Hakim faq'hi, msomi
mkubwa na mmoja wa marajii wakubwa wa Kiislamu. Alizaliwa mwaka 1264
Hijiria Shamsia. Ayatullah Hakim alipata kuhifadhi Qur'ani Tukufu akiwa
na umri mdogo na baadaye alisoma elimu ya dini kwa walimu wakubwa wa
zama zake. Msomi huyo mkubwa wa Kiislamu ameandika vitabu vingi ikiwa ni
pamoja na "Mustamsikul Urwatul Wuthqaa" chenye juzuu 14, "Haqaiqul
Usul" na "Nahjul Faqaha."
Na siku kama ya leo miaka 51
iliyopita alifariki dunia mshairi wa Kimarekani Robert Frost aliyezaliwa
mwaka 1874. Kipaji chake kikubwa katika sanaa ya mashairi kilimuwezesha
kuandika diwani yake ya kwanza ya mashairi akiwa na umri wa miaka 20.
Frost aliipa diwani hiyo ya mashairi jina la "A Boy's Will". Malenga
huyo mara kadhaa alitunukiwa tuzo ya usanii ya Pulitzer.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!