Michuano
ya kombe la dunia inataraji kuanza Juni hadi Julai, mwaka huu katika
nchini ya Brazil. Michuano hiyo itakuwa ikichezwa kwa mara ya pili
nchini humo huku mara ya mwisho ikichezwa miaka 64 wakati Uruguay
ilipotwaa ubingwa wake wa pili na wa mwisho mbele ya Brazil kwa
kuwafunga mabao 2-1 katika uwanja wa Maraccana mbele ya mashabiki
wanaokadiliwa kufikia 200, 000. Idadi kubwa zaidi ya watazamaji katika
historia ya soka. Mabingwa mara tano Brazil ndiyo wenyeji wa michuano ya
sasa. Miji 12 itaandaa michuano hiyo. Kuanzia wiki hii tutakuwa
tukiwaletea orodha ya makundi, uchambuzi na matukio muhimu yaliyowahi
kujitokeza katika michuano hiyo. Leo tutazame viwanja ambavyo
vitazipokea timu 32 ambazo zitakuwa zikiwania taji hilo.
ARENA DE SAO PAULO
Mechi sita zitachezwa katika uwanja huu uliopo mjini, Sao Paulo.
Umepewa nafasi ya kuchezwa kwa mechi ya ufunguzi itakayo husisha
wenyeji wa michuano, Brazil dhidi ya Croatia, Juni 12. Ni uwanja mpya
kabisa na utafunguliwa rasmi mapema mwaka huu. Unauwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 65, 867. Mechi nne za hatua ya makundi zitapigwa katika uwanja huu, na nyingine mbili katika hatua za mtoano.
ARENA DA BAIXADA
Ni uwanja unaoweza kuchukua watazamaji wapatao 41, 456. Upo katika mji wa Curitiba, na ulifunguliwa rasmi mwaka 1914. Mechi ya kwanza katika uwanja huu itakuwa ile kati ya Iran na Nigeria, Juni 16. Ni mechi nne
tu zitachezwa katika uwanja huu, na zote zikiwa za hatua ya makundi.
Wenyeji Brazil wanakumbukumbu mbaya na uwanja huu, walipoteza kwa mabao 2-1 mbele ya Uruguay katika fainali ya mwaka 1950. Fainali ambayo ilishuhudiwa na watu wapatao 200, 000, idadi kubwa zaidi ya watazamaji katika historia ya soka. Kwa sasa, Maracana umepunguzwa ukubwa na kufikia kuchukua idadi ya watazamaji 76, 804. Mechi ya kwanza katika uwanja huu itakuwa ni ile kati ya Argentina na Bosnia, na unatarajia kutumika katika michezo saba.
ESATADIO MINEIRAO- BELO HORIZONTE
Uwanja huu una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao, 62, 547. Ulijengwa mwaka 1965, mechi ya Colombia na Ugiriki, itakuwa ya kwanza kupigwa hapa. Mechi sita zitachezwa katika uwanja huu, nne za hatua ya makundi na mbili za hatua ya mtoano.
ESTADIO NACIONAL DE BRASILIA- BRASILIA
Uwanja huu ulifunguliwa rasmi mwaka 2012, una uwezo wa kukusanya watazamaji 66,000. Mechi ya kwanza kuchezwa katika uwanja huu ni ile ya Uswisi na Ecuador pia uwanja huu utatumika katika michezo saba sawa na ule wa Maracana. ARENA FONTE NOVA- SALVADOR
Mechi kati ya Hispania na Uholanzi itachezwa katika uwanja huu, juni 13. Ni uwanja uliofungiliwa mwaka 1951 na una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao, 48, 747. Utatumika kwa michezo sita.
ARENA PERNAMBUCANO- RECIFE
Unatarajiwa kufunguliwa mapema mwaka huu, ukiwa na uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 44, 248, Ivory Coast na Japan zinataraji kuamana hapa, juni 14. Utachezewa kwa michezo mitano, minne ya hatua ya makundi na mmoja wa hatua ya mtoano.
ESTADIO BEIRA RIO- PORTO ALEGRE
Una uwezo wa kuchukua watazamaji wapatao 48, 849 na ulifunguliwa mwaka 1969. Mechi tano zitachezwa katika uwanja huu, nne za hatua ya makundi na moja ya mtoano. Viwanja vingine ni Estadio Das Dunas, uliopo katika mji wa Natal. Uwanja huu unachukua watazamaji 42, 086, na mechi nne za hatua ya makundi zitachezwa katika uwanja huo. Pia upo Arena da Amazonia, uliopo katika mji wa Manaus
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!